Leviticus 8:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanawe Aroni nao wakaja, naye Mose akawapaka kiasi cha damu kwenye ncha za masikio yao ya kulia, vidole gumba vya mikono yao ya kulia na kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu nyingine akainyunyizia madhabahu pande zake zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia Musa akawaleta hao wana wa Haruni mbele, akaipaka sehemu ya hiyo damu kwenye ncha za masikio yao ya kuume, juu ya vidole gumba vya mikono yao ya kuume, na juu ya vidole vikubwa vya miguu yao ya kuume. Kisha akanyunyiza damu pande zote za madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya kuume, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kuume; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanawe Aroni nao wakaja, naye Mose akawapaka kiasi cha damu kwenye ncha za masikio yao ya kulia, vidole gumba vya mikono yao ya kulia na kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu nyingine akainyunyizia madhabahu pande zake zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Mose akawaleta hao wana wa Aroni mbele na kuipaka sehemu ya hiyo damu kwenye ncha za masikio yao ya kuume, juu ya vidole gumba vya mikono ya kuume na juu ya vidole vikubwa vya miguu ya kuume. Kisha akanyunyiza damu pande zote za madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia Musa akawaleta hao wana wa Haruni mbele, akaipaka sehemu ya hiyo damu kwenye ncha za masikio yao ya kuume, juu ya vidole gumba vya mikono yao ya kuume, na juu ya vidole vikubwa vya miguu yao ya kuume. Kisha akanyunyiza damu pande zote za madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya upande wa kulia, na katika vidole gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole gumba vya miguu yao ya kulia; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanawe Aroni nao wakaja, naye Mose akawapaka kiasi cha damu kwenye ncha za masikio yao ya kulia, vidole gumba vya mikono yao ya kulia na kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu nyingine akainyunyizia madhabahu pande zake zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mose akawakaribisha wanawe Haroni; nao akawapaka damu pembe za chini za masikio ya kuume na vidole gumba vya mikono yao ya kuume navyo vya miguu yao ya kuume, nayo damu nyingine Mose akainyunyizia misingi ya meza ya kutambikia pande zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya kuume, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kuume; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wana wa Haruni nao wakakuja, naye Musa akawapakaa sehemu ya damu kwenye incha za masikio yao ya kuume, vidole gumba vya mikono yao ya kuume na kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kuume. Damu ingine akainyunyizia mazabahu pande zake zote.