Leviticus 8:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, akachukua mafuta yote, mkia pamoja na mafuta yake, mafuta yote yanayofunika matumbo, sehemu bora ya ini, pamoja na figo zote mbili, mafuta yake na paja la mguu wa kulia wa nyuma wa huyo kondoo dume.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akachukua mafuta ya mnyama, mafuta ya mkia, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani, kipande kirefu cha ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, na paja la kulia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akayatwaa hayo mafuta, na mkia wenye mafuta, na mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo, na kitambi cha ini, na figo mbili, na mafuta yake, na mguu wa nyuma wa upande wa kuume;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, akachukua mafuta yote, mkia pamoja na mafuta yake, mafuta yote yanayofunika matumbo, sehemu bora ya ini, pamoja na figo zote mbili, mafuta yake na paja la mguu wa kulia wa nyuma wa huyo kondoo dume.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akachukua mafuta ya mnyama: mafuta ya mkia, mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake na paja la kulia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akachukua mafuta ya mnyama, mafuta ya mkia, mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, na paja la kulia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akayatwaa hayo mafuta, na mkia wenye mafuta, na mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo, na kitambi cha ini, na figo mbili, na mafuta yake, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, akachukua mafuta yote, mkia pamoja na mafuta yake, mafuta yote yanayofunika matumbo, sehemu bora ya ini, pamoja na figo zote mbili, mafuta yake na paja la mguu wa kulia wa nyuma wa huyo kondoo dume.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akayatwaa mafuta, ni mkia na mafuta yote yanayoshikamana na utumbo na kipande kile cha ini na mafigo yote mawili pamoja na mafuta yao na paja la kuume,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akayatwaa hayo mafuta, na mkia wenye mafuta, na mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo, na kitambi cha ini, na figo mbili, na mafuta yake, na mguu wa nyuma wa upande wa kuume;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, akatwaa mafuta yote, mukia pamoja na mafuta yake, mafuta yote yanayofunika matumbotumbo, sehemu bora ya maini, pamoja na figo zote mbili, mafuta yake na paja la muguu wa kuume wa nyuma wa huyo kondoo dume.