Leviticus 8:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akaviweka mikononi mwao Aroni na wanawe, nao wakafanya ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaviweka hivi vyote mikononi mwa Haruni na wanawe, na kuviinua mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha akaweka vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe, na kuvitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akaviweka mikononi mwao Aroni na wanawe, nao wakafanya ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaviweka hivi vyote mikononi mwa Aroni na wanawe, na kuviinua mbele za BWANA kuwa sadaka ya kuinuliwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaviweka hivi vyote mikononi mwa Haruni na wanawe, na kuviinua mbele za bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha akaweka vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe, na kuvitikisa huku na huko viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akaviweka mikononi mwao Aroni na wanawe, nao wakafanya ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akayaweka yote pia mikononi mwa Haroni namo mikononi mwa wanawe, akayapitisha motoni mbele ya Bwana, yawe vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha akaweka vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe, na kuvitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akaviweka katika mikono ya Haruni na wana wake, nao wakafanya kitambulisho cha kumutolea Yawe.