Leviticus 8:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Chemsheni ile nyama mbele ya mlango wa hema la mkutano, muile hapo mlangoni pamoja na mkate kutoka katika kikapu chenye sadaka za kuwekea wakfu. Fanyeni kama nilivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, kwamba sehemu hiyo italiwa na Aroni na wanawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Musa akamwambia Haruni na wanawe, “Pikeni hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na muile hapo pamoja na mkate kutoka kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza: ‘Haruni na wanawe wataila.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Musa akawaambia huyo Haruni na wanawe, Tokoseni hiyo nyama mlangoni pa hema ya kukutania; mkaile pale pale, na hiyo mikate iliyo katika kile kikapu cha kuwaweka wakfu, kama nilivyoagizwa kusema, Haruni na wanawe wataila.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Chemsheni ile nyama mbele ya mlango wa hema la mkutano, muile hapo mlangoni pamoja na mkate kutoka katika kikapu chenye sadaka za kuwekea wakfu. Fanyeni kama nilivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, kwamba sehemu hiyo italiwa na Aroni na wanawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Pika hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uile hapo pamoja na mkate kutoka kwenye kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza, nikisema, ‘Aroni na wanawe wataila.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Musa akamwambia Haruni na wanawe, “Pika hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na uile hapo pamoja na mkate kutoka kwenye kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza, nikisema, ‘Haruni na wanawe wataila.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Musa akawaambia huyo Haruni na wanawe, Tokoseni hiyo nyama mlangoni pa hema ya kukutania; mkaile pale pale, na hiyo mikate iliyo katika kile kikapu cha kuwaweka wakfu, kama nilivyoagizwa kusema, Haruni na wanawe wataila.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Chemsheni ile nyama mbele ya mlango wa hema la mkutano, muile hapo mlangoni pamoja na mkate kutoka katika kikapu chenye sadaka za kuwekea wakfu. Fanyeni kama nilivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, kwamba sehemu hiyo italiwa na Aroni na wanawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mose akamwambia Haroni na wanawe: Zipikeni hizi nyama hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano! Tena hapo ndipo, mtakapozila pamoja na mikate iliyomo katika kikapu cha vilaji vya tambiko vya kujaza gao, kama nilivyoagizwa kwamba: Haroni na wanawe na waile!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Musa akawaambia huyo Haruni na wanawe, Tokoseni hiyo nyama mlangoni pa hema ya kukutania; mkaile pale pale, na hiyo mikate iliyo katika kile kikapu cha kuwaweka wakfu, kama nilivyoagizwa kusema, Haruni na wanawe wataila.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akamwambia Haruni na wana wake: Mupike ile nyama mbele ya mulango wa hema la mukutano, muikulie pale kwenye mulango pamoja na mukate kutoka katika kitunga chenye sadaka za utakaso. Mufanye kama vile nilivyoamuriwa na Yawe, kwamba sehemu hiyo itakuliwa na Haruni na wana wake.