Leviticus 9:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini vile vidari na ule mguu wa nyuma wa kulia, Aroni alifanya navyo ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu, kama Mose alivyoamuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haruni akaviinua vile vidari na paja la kulia mbele za Mwenyezi Mungu ili viwe sadaka ya kuinuliwa, kama Musa alivyoagiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kuume, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya Bwana; kama Musa alivyoagiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini vile vidari na ule mguu wa nyuma wa kulia, Aroni alifanya navyo ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu, kama Mose alivyoamuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aroni akaviinua vile vidari na paja la kulia mbele za BWANA kuwa sadaka ya kuinuliwa, kama Mose alivyoagiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haruni akaviinua vile vidari na paja la kulia mbele za bwana ili viwe sadaka ya kuinuliwa, kama Musa alivyoagiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kama Musa alivyoagiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini vile vidari na ule mguu wa nyuma wa kulia, Aroni alifanya navyo ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu, kama Mose alivyoamuru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kidari na paja la kuume Haroni akavipitisha motoni huku na huko kuwa vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni mbele ya Bwana, kama Mose alivyoagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kuume, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA; kama Musa alivyoagiza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini vile vilali na ule muguu wa nyuma wa kuume, Haruni akafanya navyo kitambulisho cha kumutolea Yawe, kama vile Musa alivyoamuru.