Leviticus 9:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waambie Waisraeli wachukue beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na ndama mmoja na mwanakondoo mmoja wote wa umri wa mwaka mmoja na wasio na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha waambie Waisraeli: ‘Chukueni beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na ndama na mwana-kondoo, wote wawili wawe wa umri wa mwaka mmoja, na wasio na dosari, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utawaambia wana wa Israeli, ukisema, Twaeni mbuzi mume awe sadaka ya dhambi; na mwana-ng'ombe, na mwana-kondoo, wote wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, kwa sadaka ya kuteketezwa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waambie Waisraeli wachukue beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na ndama mmoja na mwanakondoo mmoja wote wa umri wa mwaka mmoja na wasio na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha waambie Waisraeli: ‘Chukueni mbuzi dume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, ndama na mwana-kondoo, wote wawili wawe wa umri wa mwaka mmoja, wasio na dosari, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha waambie Waisraeli: ‘Chukueni mbuzi dume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na ndama na mwana-kondoo, wote wawili wawe wa umri wa mwaka mmoja, na wasio na dosari, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utawaambia wana wa Israeli, ukisema, Twaeni mbuzi dume awe sadaka ya dhambi; na mwana-ng'ombe, na mwana-kondoo, wote wa mwaka mmoja, wakamilifu, kwa sadaka ya kuteketezwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waambie Waisraeli wachukue beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na ndama mmoja na mwanakondoo mmoja wote wa umri wa mwaka mmoja na wasio na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wana wa Isiraeli waambie kwamba: Chukueni dume la mbuzi, awe ng'ombe za tambiko ya weuo, tena ndama na mwana kondoo wa mwaka mmoja wasio na kilema, wawe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utawaambia wana wa Israeli, ukisema, Twaeni mbuzi mume awe sadaka ya dhambi; na mwana-ng’ombe, na mwana-kondoo, wote wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, kwa sadaka ya kuteketezwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie Waisraeli watwae beberu mumoja kwa ajili ya sadaka ya zambi, na mwana-ngombe mumoja na mwana-kondoo mumoja wote wa umri wa mwaka mumoja na wasiokuwa na kilema kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,