Luke 1:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini malaika akamwambia, “Zakaria, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zakaria, kwa maana Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina Yahya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Malaika akamwambia, “Usiogope, Zakaria. Mungu amelisikia ombi lako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yohana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini malaika akamwambia, “Zakariya, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini malaika akamwambia, “Zakaria, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zekaria, kwa maana Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yohana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zekaria, kwa maana Mwenyezi Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yahya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yohana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini malaika akamwambia, “Zakaria, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini malaika akamwambia: Usiogope, Zakaria! Kwani ombo lako limesikiwa: mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yohana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini yule malaika akamwambia: “Zakaria, usiogope, kwa maana Mungu amesikia maombi yako. Muke wako Elizabeti atakuzalia mutoto mwanaume, nawe utamwita jina lake Yoane.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mke wako Elizabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.