Luke 1:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakaria huku wakishangaa juu ya kukawia kwake hekaluni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo watu walikuwa wanamngojea Zakaria nje huku wakishangaa kukawia kwake mle Hekaluni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale watu walikuwa wakimngojea Zakaria, wakastaajabia kukawia kwake mle hekaluni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu waliokuwa nje ya Hekalu wakimngojea Zakaria walishangaa kwa sababu alikaa kwa muda mrefu ndani ya Hekalu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakariya huku wakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakaria huku wakishangaa juu ya kukawia kwake hekaluni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo watu walikuwa wanamngojea Zekaria nje huku wakishangaa kukawia kwake mle Hekaluni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo watu walikuwa wanamngojea Zekaria nje huku wakishangaa kukawia kwake mle Hekaluni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale watu walikuwa wakimngojea Zakaria, wakastaajabia kukawia kwake mle hekaluni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakaria huku wakishangaa juu ya kukawia kwake hekaluni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wale watu waliokuwa wakimngoja Zakaria, wakastaajabu kukawia kwake katika Jumba la Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale watu walikuwa wakimngojea Zakaria, wakastaajabia kukawia kwake mle hekaluni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa muda wote watu wale walipokuwa inje, wakimungojea Zakaria, wakashangaa kwa kuona anakawia ndani ya hekalu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wale watu walikuwa wakimugojea Zakaria, wakastaajabu kwa kukawia kwake mle hekaluni: