Luke 1:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipotoka akawa hawezi kusema nao, wao wakatambua kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Lakini kwa kuwa alikuwa bubu, akawa anawaashiria kwa mikono.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipotoka hali hawezi kusema nao, walitambua ya kuwa ameona maono ndani ya hekalu, naye aliendelea kuwaashiria akakaa bubu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Zakaria alipotoka nje hakuweza kuzungumza nao. Aliwafanyia watu ishara kwa mikono yake. Hivyo watu walitambua kuwa alikuwa ameona maono alipokuwa Hekaluni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono Hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipotoka akawa hawezi kusema nao, wao wakatambua kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Lakini kwa kuwa alikuwa bubu, akawa anawaashiria kwa mikono.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipotoka akawa hawezi kusema nao, wao wakatambua kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Lakini kwa kuwa alikuwa bubu, akawa anawaashiria kwa mikono.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipotoka akiwa hawezi kusema nao, walitambua ya kuwa ameona maono ndani ya hekalu, naye aliendelea kuwaashiria akakaa bubu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipotoka hakuweza kusema nao; ndipo, walipotambua, ya kuwa yako mambo, aliyoyaona katika Jumba la Mungu. Naye akawapungia kwa mkono, akakaa kuwa bubu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipotoka hali hawezi kusema nao, walitambua ya kuwa ameona maono ndani ya hekalu, naye aliendelea kuwaashiria akakaa bubu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipotoka inje, hakuweza kusema nao, na watu wakatambua kwamba amepata maono ndani ya hekalu. Lakini alikuwa akifanya alama kwa mikono, kwa sababu alibaki bubu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
hatta alipotoka hakuweza kusema nao, wakatambua ya kuwa ameona maono mle hekaluni; nae alikuwa akiwapungia mkouo, akadumu kuwa bubu.