Luke 1:38 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maria akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema.” Kisha yule malaika akaenda zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mariamu akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka, akamwacha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mariamu akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, basi jambo hili litokee kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maria akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema.” Kisha yule malaika akaenda zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maria akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema.” Kisha yule malaika akaenda zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maria akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa Bwana na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka akamwacha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mariamu akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka, akamwacha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maria akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema.” Kisha yule malaika akaenda zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maria akasema: Tazama, mimi ni kijakazi wa Bwana! Yaniwie, kama ulivyosema! Kisha malaika akaondoka kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Maria akasema: “Mimi ni mujakazi wa Bwana; ifanyike kwangu sawa ulivyosema.” Kisha malaika akajiendea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mariamu akasema, Tazama, mimi mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kwa neno lako. Malaika akaondoka kwake.