Luke 1:44 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nakuambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliye tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa maana sauti ya salamu yako ilipofika masikioni mwangu, mtoto aliye ndani yangu amerukaruka kwa furaha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nakwambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nakuambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nakuambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani sauti yako ya kuniamkia iliponiingia masikioni, mara kitoto tumboni mwangu kilirukaruka kwa kushangilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mara moja niliposikia salamu yako, mutoto akajitingiza kwa furaha ndani ya tumbo langu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana sauti ya salamu yako ilipoingia masikioni mwangu, mtoto mchanga aliruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.