Luke 1:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha ukuhani cha Abiya. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa utawala wa Herode mfalme wa Yudea, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, aliyekuwa wa ukoo wa kikuhani wa Abiya. Elizabeti mkewe alikuwa pia mzao wa Haruni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Herode alipokuwa mfalme wa Uyahudi, alikuwepo kuhani mmoja aliyeitwa Zakaria, aliyekuwa mmoja wa makuhani wa kikundi cha Abiya. Mkewe alikuwa mzaliwa wa ukoo wa Haruni, na jina lake alikuwa Elizabeti.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha ukuhani cha Abiya. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa Herode mfalme wa Uyahudi palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zekaria, ambaye alikuwa wa ukoo wa kikuhani wa Abiya. Elizabeti mkewe alikuwa pia mzao wa Aroni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa Herode mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zekaria, ambaye alikuwa wa ukoo wa kikuhani wa Abiya. Elizabeti mkewe alikuwa pia mzao wa Haruni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Zamani za Herode, mfalme wa Yudea, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha ukuhani cha Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha ukuhani cha Abiya. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile, Herode alipokuwa mfalme wa Wayuda, palikuwa na mtambikaji wa chama cha Abia, jina lake Zakaria, naye mkewe alikuwa na wana wa Haroni, jina lake Elisabeti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku Herode alipokuwa mufalme wa Yudea, kulikuwa kuhani mumoja, aliyeitwa Zakaria, wa kundi la makuhani wa ukoo wa Abiya. Muke wake Elizabeti alikuwa vilevile wa uzao wa Kuhani Mukubwa Haruni.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Zamani za Herode, mfalme wa Yahudi, palikuwa na kuliani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya: na mkewe alikuwa mmojawapo wa binti Haruni, jina lake Elizabeti.