Luke 1:59 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakaria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zakaria, ambalo ndilo jina la baba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtoto alipofikisha umri wa siku nane, walikuja kumtahiri. Walipotaka kumwita mtoto Zakaria kutokana na jina la baba yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakariya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakaria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zekaria, ambalo ndilo jina la baba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zekaria, ambalo ndilo jina la baba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakaria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilipokuwa siku ya nane, wakaja kumtahiri mtoto, wakamwita jina la baba yake: Zakaria.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilipotimia siku nane tangu mutoto alipozaliwa, wakaenda kumutahiri, nao wakataka kumupa jina la baba yake Zakaria.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babae, Zakaria.