Luke 1:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zakaria na Elizabeti mkewe wote walikuwa watu wanyofu mbele za Mungu, wakizishika amri zote za Mwenyezi Mungu na maagizo yote bila lawama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wote wawili Zakaria na Elizabeti walikuwa wema waliompendeza Mungu na daima walifanya yote yaliyoamriwa na Bwana na kila mara walifuata maagizo yake kwa ukamilifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zekaria na Elizabeti mkewe wote walikuwa watu wanyofu mbele za Mungu, wakizishika amri zote za Bwana na maagizo yote bila lawama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zekaria na Elizabeti mkewe wote walikuwa watu wanyofu mbele za Mwenyezi Mungu, wakizishika amri zote za Bwana Mwenyezi Mungu na maagizo yote bila lawama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiishi katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wote wawili walikuwa waongofu machoni pa Mungu, wakaendelea na kuyashika maagizo na maongozi yote ya Bwana, watu wasione la kuwaonya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote wawili walikuwa wenye haki mbele ya Mungu, walishika kwa ukamilifu amri na maagizo yote ya Bwana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao wote wawili wenye haki mbele ya Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na hukumu zake zote bila lawama.