Luke 1:65 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu, na katika nchi yote ya vilima ya Yudea watu walikuwa wakinena kuhusu mambo haya yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaingiwa na hofu wote waliokuwa wakikaa karibu nao; na mambo hayo yote yakatangazwa katika nchi yote ya milima milima ya Uyahudi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Majirani zao wakajawa hofu na watu katika sehemu zote za vilima katika jimbo la Yuda wakawa wanazungumza kuhusu jambo hili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu na katika nchi yote ya vilima vya Uyahudi watu walikuwa wakinena juu ya mambo haya yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu, na katika nchi yote ya vilima vya Uyahudi watu walikuwa wakinena juu ya mambo haya yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaingiwa na hofu wote waliokuwa wakikaa karibu nao; na mambo hayo yote yakatangazwa katika nchi yote ya Yudea yenye milima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, woga ulipowashika wote waliokaa kando kando yao; mambo hayo yote yakasimuliwa milimani po pote pa Yudea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaingiwa na hofu wote waliokuwa wakikaa karibu nao; na mambo hayo yote yakatangazwa katika nchi yote ya milima milima ya Uyahudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi watu wote waliokaa karibu naye wakashikwa na woga, na habari ya mambo haya yote ikaenea fasi zote katika inchi ya vilima vya Yudea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Khofu ikawaingia wote waliokaa karibu nao; yakaenea maneno haya pia milimani mwote Uyahudi.