Luke 10:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya hayo, Bwana aliwachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawiliwawili, wamtangulie katika kila kijiji na mahali ambapo yeye mwenyewe alitaka kwenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya hayo, Bwana Isa akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda baadaye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya hili, Bwana alichagua wafuasi sabini na wawili zaidi. Aliwatuma watangulie katika kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda wakiwa wawili wawili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya hayo, Bwana aliwachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawiliwawili, wamtangulie katika kila kijiji na mahali ambapo yeye mwenyewe alitaka kwenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya hayo, Bwana aliwachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawiliwawili, wamtangulie katika kila kijiji na mahali ambapo yeye mwenyewe alitaka kwenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya hayo, Yesu akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda yeye mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya hayo, Isa akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda baadaye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda katika kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya hayo, Bwana aliwachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawiliwawili, wamtangulie katika kila kijiji na mahali ambapo yeye mwenyewe alitaka kwenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Bwana akachagua wengine 70, akawatanguliza mbele yake wawiliwawili, waingie kila mji na kila mahali, alipotaka kwenda mwenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya maneno hayo, Bwana akawachagua watu wengine makumi saba. Naye akawatuma wawili wawili wamutangulie kupita katika kila muji na kila nafasi yeye mwenyewe alipokuwa amekusudia kwenda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BASSI baada ya mambo haya Bwana akachagua wengine sabaini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda killa mji na pahali atakakokwenda mwenyewe.