Luke 10:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia kitambo na kukaa katika majivu kutubu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani, kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ole wako, Korazini! Ole wako Bethsaida! Watu wenu wameniona nikifanya miujiza mingi ndani yenu, lakini hamkubadilika. Miujiza hiyo hiyo ingefanyika katika miji ya Tiro na Sidoni, watu katika miji hiyo wangelikwisha badili mioyo na maisha yao siku nyingi. Wangelikwisha vaa nguo za magunia na kukaa kwenye majivu kuonesha kusikitika na kutubu dhambi zao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwishavaa mavazi ya gunia kitambo, na kukaa katika majivu kuonyesha kwamba wametubu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia kitambo na kukaa katika majivu kutubu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ole wako Korazini! Ole wake Bethsaida! Kwa kuwa miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika Tiro na Sidoni, ingekuwa imetubu zamani, kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani, kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakikaa katika nguo za magunia na majivu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia kitambo na kukaa katika majivu kutubu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatakupata, wewe Korasini! Yatakupata, wewe Beti-Saida! Kwani ya nguvu yaliyofanyika kwenu kama yangalifanyika Tiro na Sidoni, wangalijuta kale na kujivika magunia na kujikalisha majivuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akaendelea kusema: “Ole kwako muji Korazini! Ole kwako muji Betesaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika ndani yenu ingefanyika katika muji wa Tiro na wa Sidona, wakaaji wa kule wangekwisha zamani kuonyesha masikitiko yao kwa kuvaa magunia na kujipakaa majivu, na kugeuka toka zambi zao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ole wako, Korazin! Ole wako Bethsaida! kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingalifanyika katika Turo na Sodom, wangalitubu zamani, wakiketi katika nguo za kigunia na majivu.