Luke 10:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka kuzimu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha! Utashushwa hadi Kuzimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nawe Kapernaumu, Je! Utatukuzwa mpaka mbinguni? Hapana, utatupwa chini hadi mahali pa kifo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na wewe Kafarnaumu, unataka kujikweza mpaka mbinguni? La; utaporomoshwa mpaka Kuzimu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka kuzimu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nawe, Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nawe, Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka kuzimu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe Kapernaumu, hukupazwa mpaka mbinguni? Utatumbukia mpaka kuzimuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nawe muji Kapernaumu, unafikiri kwamba utapandishwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka chini katika kuzimu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nawe Kapernaum, wewe uliyeinuliwa hatta mhinguni, ntashushwa hatta kuzimu.