Luke 10:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache. Kwa hivyo, mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliwaambia, “Kuna mavuno mengi ya watu wa kuwaingiza katika Ufalme wa Mungu. Lakini watenda kazi wa kuwaingiza katika ufalme wa Mungu ni wachache. Mungu anamiliki mavuno. Mwombeni ili atume watenda kazi wengi ili wasaidie kuyaingiza mavuno yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache. Kwa hivyo, mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache. Kwa hivyo, mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, awapeleke watenda kazi katika shamba lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke wafanya kazi katika mavuno yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache. Kwa hivyo, mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akawaambia: Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Mwombeni mwenye mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaambia: “Mavuno ni mengi, lakini watumishi ni wachache. Basi muombe Bwana wa mavuno atume watumishi kwa kuyavuna.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Mavuno ni mengi, illakini watenda kazi wachache; mwombeni, bassi, Bwana wa mavuno, apate kupeleka watenda kazi mavunoni mwake.