Luke 10:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akasema, “Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana atapenda kumfunulia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu. Hakuna mtu amjuaye Mwana ni nani ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ni nani ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baba yangu amenipa vitu vyote. Hakuna anayejua Mwana ni nani, Baba peke yake ndiye anayejua. Na Mwana peke yake ndiye anayejua Baba ni nani. Watu pekee watakaojua kuhusu Baba ni wale ambao Mwana amechagua kuwaambia.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akasema, “Baba yangu ameweka yote mikononi mwangu. Hakuna amjuaye Mwana ni nani ila Baba, wala amjuaye Baba ni nani ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana anataka kumfunulia hayo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akasema, “Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana atapenda kumfunulia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Vitu vyote vimekabidhiwa mkononi mwangu na Baba. Wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu. Hakuna mtu amjuaye Mwana ni nani ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ni nani ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akasema, “Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana atapenda kumfunulia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vyote nimepewa na Baba yangu. Hakuna anayemtumbua Mwana, kama ni nani, pasipo Baba; wala hakuna anayemtambua Baba, kama ni nani, pasipo Mwana, na kila, Mwana atakayemfunulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Baba yangu, umeweka vitu vyote katika mikono yangu. Hakuna mutu anayemujua Mwana isipokuwa Baba, wala hakuna anayemujua Baba isipokuwa Mwana na yeyote ambaye Mwana anataka kumujulisha kwake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawagenkia wanafunzi wake akasema, Nimekahidhiwa vyote na Baba yangu: wala hapana mtu ajuae khabari za Mwana illa Baba: wala khabari za Baha illa Mwana, na mtu ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.