Luke 10:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye mwanasheria mmoja alisimama, akamwuliza akitaka kumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uhai wa milele?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo mtaalamu mmoja wa Torati alisimama ili kumjaribu Isa, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha mwanasheria mmoja alisimama ili amjaribu Yesu. Akasema, “Mwalimu, ninatakiwa nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baadaye mwalimu mmoja wa Sheria alisimama akamwuliza akitaka kumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye mwanasheria mmoja alisimama, akamwuliza akitaka kumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uhai wa milele?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate kurithi uzima wa milele?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Isa, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, mwanasheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye mwanasheria mmoja alisimama, akamwuliza akitaka kumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uhai wa milele?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pakawapo mjuzi wa Maonyo, akainuka, akamtega akisema: Mfunzi, nifanye nini, nipate kuurithi uzima wa kale na kale?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mwalimu mumoja wa Sheria akasimama na kumwuliza Yesu kwa kumupima: “Mwalimu, nifanye nini kusudi nipate uzima wa milele?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwana sharia mmoja akasimama akimjaribu, akasema, Mwalimu, nifanyeni niurithi uzima wa milele?