Luke 10:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini yeye akitaka kujihakikishia kuwa mwema akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yule mtaalamu wa Torati, akitaka kujionesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Isa, “Jirani yangu ni nani?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mwanasheria alitaka kuonesha kuwa alikuwa mwenye haki na aliishi kwa usahihi. Hivyo akamwuliza Yesu, “Lakini si kila mtu aliye jirani yangu, au unasemaje?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini yeye akitaka kujihakikishia kuwa mwema akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini yeye akitaka kujihakikishia kuwa mwema akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini yule mtaalamu wa sheria akitaka kuonyesha kuwa mwenye haki, akamwuliza Yesu, “Jirani yangu ni nani?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yule mtaalamu wa Torati, akitaka kujionyesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Isa, “Jirani yangu ni nani?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini yeye akitaka kujihakikishia kuwa mwema akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwa sababu alitaka kujijulisha kuwa ni mwongofu, akamwambia Yesu: Mwenzangu ni nani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa kutaka kujipatia haki, yeye akamwuliza Yesu: “Mwenzangu ni nani?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae akitaka kujifanya ana haki akamwambia Yesu, Na jirani yangu ni nani?