Luke 10:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona, akapita kando.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani mmoja alikuwa akipitia njia ile, alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikatokea kuwa kuhani mmoja alikuwa anasafiri kupitia njia hiyo hiyo. Alipomwona, hakusimama ili amsaidie, alikwenda zake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona, akapita kando.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona, akapita kando.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa bahati nzuri kuhani mmoja alikuwa anapitia njia ile, alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani mmoja alikuwa akipitia njia ile, alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona, akapita kando.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikatukia, mtambikaji akiitelemkia njia ile; alipomwona akaepuka, akapita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kukatokea kuhani mumoja akishuka katika njia ile ile. Wakati alipomwona yule mutu, akapita pembeni na kujiendea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kwa nasibu kukashuka kuhani mmoja njia ileile, akamwona, akapita upande.