Luke 10:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akamwendea, akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai na kuyafunga; halafu akampandisha juu ya punda wake, akampeleka katika nyumba moja ya wageni akamwuguza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaenda alipokuwa na akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, kisha akayafunga. Ndipo akampandisha kwenye punda wake, akampeleka hadi kwenye nyumba ya wageni na kumtunza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alimkaribia ili amsaidie, akamsafisha majeraha kwa mafuta ya zeituni na divai, kisha akayafunga majeraha yake. Msamaria alikuwa na punda. Akampandisha juu ya punda wake na kumpeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni. Akamhudumia huko.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akamwendea, akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai; na kuyafunga halafu akampandisha juu ya punda wake akampeleka katika nyumba moja ya wageni akamuuguza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akamwendea, akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai na kuyafunga; halafu akampandisha juu ya punda wake, akampeleka katika nyumba moja ya wageni akamwuguza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akamwendea, akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, kisha akayafunga. Ndipo akampandisha kwenye punda wake akamleta mpaka kwenye nyumba ya wageni na kumtunza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaenda alipokuwa na akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, kisha akayafunga. Ndipo akampandisha kwenye punda wake, akampeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni na kumtunza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akakaribia, akamfunga majeraha yake, akayatia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akamwendea, akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai na kuyafunga; halafu akampandisha juu ya punda wake, akampeleka katika nyumba moja ya wageni akamwuguza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamjia, akamfunga madonda yake akiyamwagia mafuta na mvinyo, akampandisha juu ya punda wake yeye mwenyewe, akampeleka kifikioni, akamwuguza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akajongea karibu naye, akamutunza vidonda, akivimwangia divai na kuvimimia mafuta na kuvifunga na vitambaa. Kisha akamupandisha juu ya punda wake, na kumupeleka kwenye nyumba ya kupangisha wageni na kumuchunga.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bassi akamjongelea, akamfunga jeraha zake, akitia mafuta na mvinyo: akampandisha juu ya nyama wake, akamleta katika nyumba ya wageni, akamwuguza.