Luke 10:35 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake akatoa fedha dinari mbili akampa yule mwenye nyumba, akamwambia, ‘Mwuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa nitakaporudi.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kesho yake, yule Msamaria akachukua dinari mbili akampa yule mwenye nyumba ya wageni na kusema, ‘Mtunze, nami nirudipo nitakulipa gharama yoyote ya ziada uliyotumia kwa ajili yake.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku iliyofuata, Msamaria alitoa sarafu mbili za fedha na kumpa mtunza nyumba ya wageni, akamwambia, ‘Mtunze mtu huyu aliyejeruhiwa. Ukitumia pesa nyingi zaidi kwa kumhudumia, nitakulipa nitakapokuja tena.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kesho yake akatoa fedha dinari mbili akampa yule mwenye nyumba, akamwambia, Muuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa nitakaporudi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake akatoa fedha dinari mbili akampa yule mwenye nyumba, akamwambia, ‘Mwuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa nitakaporudi.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kesho yake, yule Msamaria akachukua dinari mbili akampa yule mwenye nyumba ya wageni na kusema, ‘Mtunze, nami nirudipo nitakulipa gharama yo yote ya ziada uliyotumia kwa ajili yake.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kesho yake, yule Msamaria akachukua dinari mbili akampa yule mwenye nyumba ya wageni na kusema, ‘Mtunze, nami nirudipo nitakulipa gharama yoyote ya ziada uliyotumia kwa ajili yake.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na chochote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake akatoa fedha dinari mbili akampa yule mwenye nyumba, akamwambia, ‘Mwuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa nitakaporudi.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya kesho akatoa shilingi mbili, akampa mwenye fikio, akasema: Mwuguze huyu! Kama unatumia kuzipita hizi, nitakulipa zote nitakaporudi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake akatwaa vikoroti viwili vya feza, na kuvitoa kwa mwenye nyumba, akimwambia: ‘Umuchunge mutu huyu, na feza zingine utakazotumia zaidi ya hizi kwa matunzo yake, nitazilipa kwako nitakaporudia.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta assubuhi yake akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba, akasema, Mwuguze: na cho chote utakachogharimia zaidi, nirudipo, nitakulipa.