Luke 10:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama akiwako mpenda amani, amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama kuna mtu wa amani humo, basi amani yenu itakuwa juu yake. La sivyo, itawarudia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa watu wanaoishi katika nyumba hiyo wanapenda amani, baraka yenu ya amani itakaa nao. Lakini kama siyo, baraka yenu ya amani itawarudia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama akiwako mwenye kupenda amani, amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama akiwako mpenda amani, amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama kuna mtu wa amani humo, basi amani yenu itakuwa juu yake, la sivyo itawarudia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama kuna mtu wa amani humo, basi amani yenu itakuwa juu yake. La sivyo, itawarudia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; lakini kama hamna, amani yenu itarudi kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama akiwako mpenda amani, amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakapokuwa, yumo mwenye kutengemana, utengemano wenu utamkalia. Lakini kama hatakuwamo, utawarudia ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mule mukiwa mutu anayekuwa tayari kupokea amani, atakaa na amani ile muliyomutakia. Kama si vile, amani ile itawarudilia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kama yumo mwana wa amani, amani yenu itakaa kwake. La! si hivyo, itawarudia ninyi.