Luke 10:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa wanavyowapeni, maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msiende mara nyumba hii mara nyumba ile.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kaeni katika nyumba hiyo, mkila na kunywa kile watakachowapa, kwa sababu kila mtendakazi anastahili malipo yake. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kaeni katika nyumba inayopenda amani. Kuleni na kunywa chochote watakachowapa kwa maana mfanyakazi anastahili ujira. Msihame kutoka katika nyumba hiyo na kwenda kukaa katika nyumba nyingine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa wanavyowapeni, maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msiende mara nyumba hii mara nyumba ile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa wanavyowapeni, maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msiende mara nyumba hii mara nyumba ile.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kaeni katika nyumba hiyo, mkila na kunywa kile watakachowapa, kwa sababu kila mtenda kazi anastahili malipo yake. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kaeni katika nyumba hiyo, mkila na kunywa kile watakachowapa, kwa sababu kila mtendakazi anastahili malipo yake. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kaeni katika nyumba hiyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtendakazi amestahili kupewa ujira wake. Msihamehame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa wanavyowapeni, maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msiende mara nyumba hii mara nyumba ile.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo nyumbani mlemle mkaeni mkila, mkinywa mnavyopewa! Kwani mtenda kazi hupaswa na kupewa mshahara wake. Msizunguke nyumba kwa nyumba!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukae ndani ya nyumba ile, nanyi mukule na kunywa chochote watakachowapa, kwa maana mutumishi anastahili kupewa mushahara wake. Musihame nyumba kwa nyumba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kaeni katika nyumba hiyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; kwa maana mtenda kazi astahili kupewa ijara yake.