Luke 11:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini yeye, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, “Ufalme wowote uliogawanyika vikundi vinavyopingana hauwezi kudumu; kadhalika, jamaa yoyote iliyo na mafarakano huangamia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akajua mawazo yao, naye akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Nayo nyumba iliyogawanyika dhidi yake yenyewe itaanguka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akajua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini alijua walichokuwa wanafikiria, hivyo akawaambia, “Kila ufalme unaopigana wenyewe huteketezwa; na familia yenye magomvi husambaratika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini yeye, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, “Ufalme wowote uliofarakana wenyewe, hauwezi kudumu; kadhalika, jamaa yeyote inayofarakana huangamia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini yeye, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, “Ufalme wowote uliogawanyika vikundi vinavyopingana hauwezi kudumu; kadhalika, jamaa yoyote iliyo na mafarakano huangamia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia, nayo nyumba iliyogawanyika dhidi yake yenyewe huanguka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akajua mawazo yao, naye akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Nayo nyumba iliyogawanyika dhidi yake yenyewe itaanguka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akajua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini yeye, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, “Ufalme wowote uliogawanyika vikundi vinavyopingana hauwezi kudumu; kadhalika, jamaa yoyote iliyo na mafarakano huangamia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuyajua hayo mawazo yao, akawaambia: Kila ufalme unapogombana wao kwa wao huwa mahame tu, nazo nyumba huangukiana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akajua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini yeye akiwa anatambua mawazo yao, akawaambia: “Watu wa ufalme wowote wakigombana wao kwa wao, ufalme ule utaanguka. Na watu wa jamaa moja wakigombana wao kwa wao, jamaa ile itaanguka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae, akiyajua mawazo yao, akawaambia, Killa ufalme uliogawanyika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa, na nyumba iliyogawanyika nyumba kwa nyumba huanguka.