Luke 11:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama Shetani anajipinga mwenyewe, utawala wake utasimamaje? Mnasemaje, basi, kwamba ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama Shetani amegawanyika mwenyewe, ufalme wake utasimamaje? Nawaambia haya kwa sababu ninyi mnadai ya kuwa mimi ninatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, ikiwa Shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo, ikiwa Shetani anapigana yeye mwenyewe, ufalme wake utasimamaje? Ninawauliza hivi kwa kuwa mnasema kwamba ninatoa pepo kwa kutumia nguvu za Shetani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama Shetani anajipinga mwenyewe, utawala wake utasimamaje? Mnasemaje, basi, kwamba ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama Shetani anajipinga mwenyewe, utawala wake utasimamaje? Mnasemaje, basi, kwamba ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama Shetani amegawanyika mwenyewe ufalme wake utasimamaje? Nawaambia haya kwa sababu ninyi mnadai ya kuwa mimi ninatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama Shetani amegawanyika mwenyewe, ufalme wake utasimamaje? Nawaambia haya kwa sababu ninyi mnadai ya kuwa mimi ninatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, ikiwa Shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama Shetani anajipinga mwenyewe, utawala wake utasimamaje? Mnasemaje, basi, kwamba ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Satani anapojigombanisha mwenyewe, ufalme wake utasimamikaje? Kwani mnasema: Nafukuza pepo kwa nguvu ya Belzebuli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, ikiwa Shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi ikiwa Shetani akijigombanisha mwenyewe, ufalme wake hautadumu. Ninasema hivi, kwa maana ninyi munasema kama ninafukuza pepo kwa uwezo wa Belzebuli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae Shetani vivyo hivyo akigawanyika katika nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? kwa maana ninyi mnasema ninafukukuza pepo kwa Beelzebul.