Luke 11:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama ninafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, wafuasi wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo, wao ndio watakaowahukumu nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mimi natoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu nao je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao ndio watakaowahukumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kama mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, wana wenu je! Huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo, hao ndio watakaowahukumu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ikiwa ninatoa pepo kwa kutumia nguvu za Shetani, watu wenu wanatumia nguvu gani wanapotoa pepo? Hivyo watu wenu wenyewe watathibitisha kuwa ninyi ni waovu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama ninafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, watoto wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo, wao ndio watakaowahukumu ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama ninafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, wafuasi wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo, wao ndio watakaowahukumu nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao watakuwa mahakimu wenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mimi natoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu nao je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao ndio watakaowahukumu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kama mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, wana wenu je! Huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo, hao ndio watakaowahukumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama ninafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, wafuasi wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo, wao ndio watakaowahukumu nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nikiwafukuza pepo kwa nguvu ya Belzebuli, Je? Wana wenu huwafukuza kwa nguvu ya nani? Kwa hiyo hao ndio watakaowaumbua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kama mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, wana wenu je! Huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo, hao ndio watakaowahukumu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena ikiwa ninafukuza pepo kwa uwezo wa Belzebuli, basi watu wa kikundi chenu wanawafukuza kwa uwezo wa nani? Watu hao watashuhudia kwa njia ya matendo yao kwamba ninyi ni wakosaji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini mimi nikifukuza pepo kwa Beelzebul, wana wenu huwafukuza kwa nani? bassi kwa hiyo hawo ndio watakaokuwa waamuzi wenu.