Luke 11:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini akija mwenye nguvu zaidi akamshambulia na kumshinda, huyo huziteka silaha zake alizotegemea na kugawanya nyara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye akimshambulia na kumshinda, yeye humnyang’anya silaha zake zote alizozitegemea, na kuchukua nyara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang'anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini chukulia kuwa mwenye nguvu zaidi kuliko yeye akimshambulia na kumshinda, yule mwenye nguvu zaidi humnyang'anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea kuilinda nyumba yake. Ndipo mwenye nguvu zaidi atavitumia vitu vya yule mtu wa kwanza kadri anavyotaka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini akija mwenye nguvu zaidi akamshambulia na kumshinda, huyo huziteka silaha zake alizotegemea na kugawanya nyara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini akija mwenye nguvu zaidi akamshambulia na kumshinda, huyo huziteka silaha zake alizotegemea na kugawanya nyara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mtu mwenye nguvu zaidi kuliko yeye amshambuliapo na kumshinda, humnyang'anya silaha zake zote alizozitegemea na kuchukua nyara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mtu mwenye nguvu zaidi kumliko akimshambulia na kumshinda, yeye humnyang’anya silaha zake zote alizozitegemea, na kuchukua nyara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang'anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini akija mwenye nguvu zaidi akamshambulia na kumshinda, huyo huziteka silaha zake alizotegemea na kugawanya nyara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mwenye nguvu kuliko yeye atakapomjia na kumshinda atamnyang'anya mata yake yote yaliyomshikiza, kisha atayagawanya mateka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang’anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mutu mwingine mwenye nguvu zaidi akimushambulia na kumushinda, anamunyanganya silaha zake alizotegemea na kugawanya vitu vya unyanganyi anavyokuwa navyo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
lakini mwenye nguvu za kumpita yeye atakapokuja na kumshinda, amnyangʼanya silaha zake zote alizotegemea, na mateka yake ayagawanya.