Luke 11:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu, huzururazurura jangwani kukavu akitafuta mahali pa kupumzika. Asipopata, hujisemea: ‘Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Pepo mchafu anapomtoka mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu anapotokwa na roho chafu, roho hiyo husafiri sehemu zilizo kavu, ikitafuta mahali ili ipumzike. Lakini hukosa mahali pa kupumzika. Hivyo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba nilikotoka.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu fulani, huzururazurura jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata, hujisemea: Nitarudi kwenye makao yangu nilikotoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu, huzururazurura jangwani kukavu akitafuta mahali pa kupumzika. Asipopata, hujisemea: ‘Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Pepo mchafu amtokapo mtu, huzungukazunguka sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini asipopata mahali po pote husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Pepo mchafu amtokapo mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu, huzururazurura jangwani kukavu akitafuta mahali pa kupumzika. Asipopata, hujisemea: ‘Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pepo mchafu anapomtoka mtu hupita mahali pasipo na maji akitafuta kituo. Asipokiona husema: Nitarudi nyumbani mwangu, nilimotoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Wakati pepo amekwisha kutoka ndani ya mutu, anazungukazunguka kwenye ukiwa katika jangwa akitafuta nafasi ya kupumzikia. Asipopata nafasi ile, anasema: ‘Nitarudia ndani ya nyumba yangu nilimotoka.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Pepo mchafu amtokapo mtu, hupita kati ya mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika: asipopata hunena, Nitarudi uyumbani kwangu nilikotoka.