Luke 11:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu, akasema kwa sauti kubwa: “Heri mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikawa Isa alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katikati ya umati ule wa watu akapaza sauti akasema, “Limebarikiwa tumbo lililokuzaa na matiti uliyonyonya!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alipokuwa akisema mambo haya, mwanamke mmoja katika kundi la watu akapaza sauti akamwambia “Amebarikiwa na Mungu mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu, akasema kwa sauti kubwa: “Heri tumbo lililokuzaa, na maziwa yaliyokunyonyesha!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu, akasema kwa sauti kubwa: “Heri mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa Yesu alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katikati ya ule umati wa watu akapaza sauti akasema, “Limebarikiwa tumbo lililokuzaa na matiti uliyonyonya!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa Isa alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katikati ya ule umati wa watu akapaza sauti akasema, “Limebarikiwa tumbo lililokuzaa na matiti uliyonyonya!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu, akasema kwa sauti kubwa: “Heri mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, alipoyasema haya, mwanamke aliyekuwako katika kundi la watu akapaza sauti akimwambia: Lenye shangwe ni tumbo lililokuzaa na maziwa, uliyoyanyonya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamuke mumoja kati ya kundi la watu akasema kwa sauti kubwa: “Heri mwanamuke yule aliyekuzaa na kukunyonyesha!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa alipokuwa akinena haya, mwauamke mmoja katika makutano akapaaza sauti yake akamwambia, Li kheri tumbo lililokuehukua, na maziwa uliyonyonya.