Luke 11:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni na kumbe hapa pana mkuu kuliko Solomoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kuwahukumu watu wa kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Sulemani. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku ya hukumu, ninyi watu mnaoishi sasa, mtalinganishwa na Malkia wa Kusini, naye pia, atakuwa shahidi atakayeonyesha namna mlivyo waovu. Kwa nini ninasema haya? Kwa sababu alisafiri kutoka mbali, mbali sana ili ayasikilize mafundisho yenye hekima ya Suleimani. Na ninawaambia mkuu kuliko Suleimani yupo hapa, lakini hamnisikilizi!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atashuhudia kwamba kina hatia. Yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni; kumbe hapa pana mkuu zaidi kuliko Solomoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni na kumbe hapa pana mkuu kuliko Solomoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya hukumu, Malkia wa Kusini atainuka pamoja na watu wa kizazi hiki akiwahukumu kwa sababu yeye alisafiri kutoka mbali kuja kusikiliza hekima ya Solomoni. Lakini sasa, yeye aliye mkuu kuliko Solomoni yuko hapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kuwahukumu watu wa kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Sulemani. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni na kumbe hapa pana mkuu kuliko Solomoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mfalme wa kike aliyetoka kusini atawainukia waume wa ukoo huu siku ya hukumu, awaumbue. Kwani yeye alitoka mapeoni kwa nchi, aje kuusikia werevu wa Salomo uliokuwa wa kweli. Tena tazameni, hapa yupo anayempita Salomo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile kwa Siku ya hukumu, Malkia toka Kusini atasimama na watu wa kizazi hiki na kuwashitaki, kwa sababu yeye alitoka mbali sana kuja kusikiliza maneno ya hekima ya mufalme Solomono. Hapa kuna yule anayekuwa mukubwa kupita Solomono!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malkia wa kusini atafufuliwa siku ile ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atawahukumu; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia illi kuisikia hekima ya Sulemani; na hapa pana khabari kubwa kuliko Sulemani.