Luke 11:32 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Ninewi watatokea wakati wa hukumu, nao watakihukumu kizazi hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona; na kumbe hapa pana kikuu kuliko Yona!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya hukumu, watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku ya hukumu, ninyi watu mnaoishi sasa mtafananishwa pia na watu wa Ninawi, nao watakuwa mashahidi watakaoonyesha makosa yenu. Ninasema hivi kwa sababu Yona alipowahubiri, walibadili mioyo na maisha yao. Na sasa mnamsikia mtu aliye mkuu kuliko Yona, Lakini hamtaki kubadilika!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wa Ninewi watatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, na watashuhudia kwamba kizazi hiki kina hatia. Hao watu wa Ninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona; na hapa pana mkuu zaidi kuliko Yona!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Ninewi watatokea wakati wa hukumu, nao watakihukumu kizazi hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona; na kumbe hapa pana kikuu kuliko Yona!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ile ya hukumu, watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu kwa sababu wao walitubu walipomsikia Yona akihubiri. Lakini sasa, yeye aliye mkuu kuliko Yona yuko hapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya hukumu, watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Ninewi watatokea wakati wa hukumu, nao watakihukumu kizazi hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona; na kumbe hapa pana kikuu kuliko Yona!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya hukumu waume wa Niniwe watauinukia ukoo huu, wauumbue; kwani walijuta kwa tangazo la Yona. Tena tazameni, hapa yupo anayempita Yona!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa Siku ya hukumu, watu wa Ninawe watasimama nanyi watu wa kizazi hiki na kuwashitaki, kwa sababu wao waligeuka toka zambi zao waliposikia mahubiri ya Yona! Hapa kuna yule anayekuwa mukubwa kupita Yona!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Watu wa Ninawi watasimama siku ile ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao wataihukumu: maana wao walitubu kwa ajili ya makhubiri ya Yunus, na hapa pana khabari kubwa kuliko Yunus.