Luke 11:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa debe, bali huiweka juu ya kinara ili watu wanaoingia ndani wapate kuona mwanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hakuna mtu yeyote awashaye taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunikia chini ya bakuli. Badala yake huiweka juu ya kinara chake, ili watu wote wanaoingia waone nuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna mtu anayechukua taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunika. Badala yake huiweka mahali palipo wazi, ili wanaoingia ndani waweze kuiona nuru yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa pishi, bali huiweka juu ya kinara ili watu wanaoingia ndani wapate kuona mwanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa debe, bali huiweka juu ya kinara ili watu wanaoingia ndani wapate kuona mwanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hakuna mtu ye yote awashaye taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunikia chini ya bakuli. Badala yake huiweka juu ya kinara chake, ili watu wote wanaoingia waone nuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hakuna mtu yeyote awashaye taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunikia chini ya bakuli. Badala yake huiweka juu ya kinara chake, ili watu wote wanaoingia waone nuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa debe, bali huiweka juu ya kinara ili watu wanaoingia ndani wapate kuona mwanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakuna mwenye kuwasha taa anayeiweka panapofichika au chini ya kapu, ila huiweka juu ya mwango, maana wanaoingia waone mwanga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hakuna mutu anayewakisha taa na kuificha au kuifunika na kitunga; lakini anaiweka juu ya kinara kusudi wanaoingia ndani wapate kuona mwangaza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hapana mtu awashae taa na kuiweka mahali pa siri au chini va pishi, bali huiweka juu ya kibao cha kuwekea taa: illi waingiao wanone mwanga.