Luke 11:43 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ole wenu nyinyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kuketi mbele mahali pa heshima katika masunagogi, na kusalimiwa kwa heshima hadharani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ole wenu Mafarisayo, kwa sababu ninyi mnapenda kukalia viti vya mbele katika masinagogi, na kusalimiwa kwa heshima masokoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ole wenu ninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kupata viti vya heshima katika masinagogi. Na mnapenda kusalimiwa na watu kwa kuheshimiwa sehemu za masoko.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ole wenu ninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kuketi mbele mahali pa heshima katika masunagogi, na kusalimiwa kwa heshima hadharani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ole wenu nyinyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kuketi mbele mahali pa heshima katika masunagogi, na kusalimiwa kwa heshima hadharani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ole wenu Mafarisayo, kwa sababu ninyi mnapenda kuketi viti vya mbele katika masinagogi na kusalimiwa kwa heshima masokoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ole wenu Mafarisayo, kwa sababu ninyi mnapenda kukalia viti vya mbele katika masinagogi, na kusalimiwa kwa heshima masokoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ole wenu nyinyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kuketi mbele mahali pa heshima katika masunagogi, na kusalimiwa kwa heshima hadharani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatawapata, ninyi Mafariseo, kwani nyumbani mwa kuombea mnapenda viti vya mbele, tena hupenda kuamkiwa na watu sokoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ole kwenu, ninyi Wafarisayo! Munapenda kuikaa katika viti vya mbele ndani ya nyumba ya kuabudia na kusalimiwa kwa heshima kwenye nafasi za makutano.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ole wenu, Mafarisayo, kwa sababu mwapenda kukaa mbele katika sunagogi na kusalimiwa masokoni.