Luke 11:46 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamjibu, “Na nyinyi waalimu wa sheria, ole wenu; maana mnawatwika watu mizigo isiyochukulika, huku nyinyi wenyewe hamnyoshi hata kidole kuwasaidia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamjibu, “Nanyi wataalamu wa Torati, ole wenu, kwa sababu mnawatwika watu mizigo mizito ambayo hawawezi kubeba, wala ninyi wenyewe hamwinui hata kidole kimoja kuwasaidia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Nanyi wana-sheria, ole wenu, kwa sababu mwawatwika watu mizigo isiyochukulika, wala ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kimoja cha vidole vyenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akamjibu, “Ole wenu, enyi wanasheria! Mnatunga sheria kali ambazo ni vigumu watu kuzitii. Mnawalazimisha wengine kuzitii sheria zenu. Lakini ninyi wenyewe hamthubutu hata kujaribu kufuata mojawapo ya sheria hizo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamjibu, “Na ninyi walimu wa Sheria, ole wenu; maana mnawatwika watu mizigo isiyochukulika, huku ninyi wenyewe hamnyoshi hata kidole kuwasaidia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamjibu, “Na nyinyi waalimu wa sheria, ole wenu; maana mnawatwika watu mizigo isiyochukulika, huku nyinyi wenyewe hamnyoshi hata kidole kuwasaidia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamjibu, “Nanyi wataalamu wa sheria, ole wenu, kwa sababu mnawatwika watu mizigo mizito ambayo hawawezi kubeba, wala ninyi wenyewe hamwinui hata kidole kimoja kuwasaidia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamjibu, “Nanyi wataalamu wa Torati, ole wenu, kwa sababu mnawatwika watu mizigo mizito ambayo hawawezi kubeba, wala ninyi wenyewe hamwinui hata kidole kimoja kuwasaidia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Nanyi wanasheria, ole wenu, kwa sababu mwawatwika watu mizigo isiyochukulika, wala ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kimoja cha vidole vyenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamjibu, “Na nyinyi waalimu wa sheria, ole wenu; maana mnawatwika watu mizigo isiyochukulika, huku nyinyi wenyewe hamnyoshi hata kidole kuwasaidia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akasema: Nanyi wajuzi wa Maonyo yatawapata, kwani mnatwika watu mizigo isiyochukulika, nanyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kidole chenu kimoja tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Nanyi wana-sheria, ole wenu, kwa sababu mwawatwika watu mizigo isiyochukulika, wala ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kimoja cha vidole vyenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akajibu: “Ole kwenu vilevile, ninyi walimu wa Sheria! Munawabebesha watu mizigo mizito, lakini ninyi wenyewe hamufikiri hata kidogo juu ya namna ya kuwasaidia kuibeba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Na ninyi wana sharia, ole wenu, kwa sababu mwawachukuza watu mizigo isiyochukulika, na ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo kwa kimojawapo cha vidole vyenu.