Luke 11:52 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ole wenu nyinyi waalimu wa sheria, kwa sababu mmeuficha ule ufunguo wa mlango wa elimu; nyinyi wenyewe hamkuingia na mmewazuia waliokuwa wanaingia wasiingie.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ole wenu ninyi wataalamu wa Torati, kwa sababu mmeuondoa ufunguo wa maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ole wenu, ninyi wanasheria, mmechukua ufunguo wa kujifunza kuhusu Mungu. Ninyi wenyewe hamtaki kujifunza na mmewazuia wengine wasijifunze pia.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ole wenu ninyi walimu wa Sheria, kwa sababu mmeuficha ule ufunguo wa mlango wa elimu; ninyi wenyewe hamkuingia na mmewazuia waliokuwa wanaingia wasiingie.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ole wenu nyinyi waalimu wa sheria, kwa sababu mmeuficha ule ufunguo wa mlango wa elimu; nyinyi wenyewe hamkuingia na mmewazuia waliokuwa wanaingia wasiingie.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ole wenu ninyi wataalamu wa sheria, kwa sababu mmeuondoa ufunguo wa maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ole wenu ninyi wataalamu wa Torati, kwa sababu mmeuondoa ufunguo wa maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wenu, enyi wanasheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ole wenu nyinyi waalimu wa sheria, kwa sababu mmeuficha ule ufunguo wa mlango wa elimu; nyinyi wenyewe hamkuingia na mmewazuia waliokuwa wanaingia wasiingie.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatawapata, ninyi wajuzi wa Maonyo, kwani mliutwaa ufunguo wa utambuzi; wenyewe hamkuingia, mkawazuia wao waliotaka kuingia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ole kwenu, ninyi walimu wa Sheria! Mumewaficha watu ufunguo wasiingie kwenye nafasi wanapoweza kujifunza elimu. Ninyi wenyewe hamuingii pale, nanyi munawazuia wale wanaotaka kuingia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ole wenu, enyi wana sharia, kwa sababu mliuchukua ufunguo wa maarifa; ninyi wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mliwazuia.