Luke 11:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye, akiwa ndani angemjibu: ‘Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kisha yule aliye ndani amjibu, ‘Usinisumbue. Mlango umefungwa, nami na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka nikupe chochote.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Rafiki yako ndani ya nyumba akajibu, ‘Nenda zako! Usinisumbue! Mlango umefungwa. Mimi na watoto wangu tumeshapanda kitandani kulala. Siwezi kuamka ili nikupe kitu chochote kwa sasa.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye, akiwa ndani angemjibu: Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye, akiwa ndani angemjibu: ‘Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kisha yule aliyeko ndani amjibu, ‘Usinisumbue. Mlango umefungwa, nami na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka nikupe cho chote.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kisha yule aliyeko ndani amjibu, ‘Usinisumbue. Mlango umefungwa, nami na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka nikupe chochote.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na yule wa ndani amjibu akisema, Usinisumbue; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kutoka nikupe?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye, akiwa ndani angemjibu: ‘Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, kwenu yule wa ndani atamjibu nini? Atamwambia: Usinisumbue! Kwani mlango umekwisha fungwa, nao watoto wangu wako kitandani pamoja nami; siwezi kuinuka, nikupe?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na yule anayekuwa ndani ya nyumba akimujibu: ‘Usiniuzi! Mulango umekwisha kufungwa. Mimi na watoto wangu tumekwisha kulala; siwezi kuamuka kwa kukupatia mikate.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na yule mle ndani akamjibu, akimwambia, Usiniudhi: mlango umekwisha kufungwa, na watoto wangu wamelala pamoja nami kitandani; siwezi kuondoka nikupe.