Luke 12:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitafanya hivi: Nitabomoa ghala zangu na kujenga kubwa zaidi, nami nitahifadhi humo mavuno yangu yote na mali yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ndipo huyo tajiri akasema, ‘Nitafanya hivi: Nitabomoa maghala yangu ya nafaka na kujenga mengine makubwa zaidi na nihifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akasema, ‘Ninajua nitakachofanya. Nitabomoa ghala zangu na kujenga ghala kubwa zaidi! Nitahifadhi nafaka zangu zote na vitu vingine vizuri katika ghala zangu mpya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nitafanya hivi: nitabomoa ghala zangu na kujenga kubwa zaidi, na humo nitahifadhi mavuno yangu yote na mali yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitafanya hivi: nitabomoa ghala zangu na kujenga kubwa zaidi, nami nitahifadhi humo mavuno yangu yote na mali yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ndipo huyo tajiri akasema, ‘Nitafanya hivi: Nitabomoa ghala zangu za nafaka na kujenga nyingine kubwa zaidi na huko nitayahifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ndipo huyo tajiri akasema, ‘Nitafanya hivi: Nitabomoa ghala zangu za nafaka na kujenga nyingine kubwa zaidi na huko nitayahifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitafanya hivi: Nitabomoa ghala zangu na kujenga kubwa zaidi, nami nitahifadhi humo mavuno yangu yote na mali yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akasema: Nitafanya hivyo: nitayavunja mawekeo yangu, nijenge makubwa kuyapita hayo ndimo niziweke ngano zangu na mali zangu zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akajisemesha: ‘Nitafanya hivi: nitabomoa gala zangu na nitajenga zingine kubwa zaidi, na mule nitaweka mavuno yangu yote na mali zangu zingine.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Nitafanya hivi: nitavunja ghala zangu, nitajenga kubwa zaidi: na humo nitaweka akiba nafaka zangu zote, na mali zangu.