Luke 12:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chukueni kwa mfano, kunguru: Hawapandi, hawavuni wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Mungu huwalisha. Nyinyi mna thamani zaidi kuliko ndege!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Fikirini ndege! Wao hawapandi wala hawavuni, hawana ghala wala popote pa kuhifadhi nafaka; lakini Mungu huwalisha. Ninyi ni wa thamani kuliko ndege!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, na Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waangalieni kunguru, hawapandi, hawavuni au kuweka katika majumba au ghala, lakini Mungu huwalisha. Ninyi ni wa thamani sana kuliko ndege.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Chukueni kwa mfano, kunguru: hawapandi, hawavuni wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Mungu huwalisha. Ninyi mna thamani zaidi kuliko ndege!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Chukueni kwa mfano, kunguru: hawapandi, hawavuni wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Mungu huwalisha. Nyinyi mna thamani zaidi kuliko ndege!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Fikirini ndege! Wao hawapandi wala hawavuni, hawana ghala wala po pote pa kuhifadhi nafaka, lakini Mungu huwalisha. Ninyi ni bora kuliko ndege!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Fikirini ndege! Wao hawapandi wala hawavuni, hawana ghala wala popote pa kuhifadhi nafaka; lakini Mungu huwalisha. Ninyi ni wa thamani zaidi kuliko ndege!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, lakini Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chukueni kwa mfano, kunguru: Hawapandi, hawavuni wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Mungu huwalisha. Nyinyi mna thamani zaidi kuliko ndege!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jifundisheni kwa makunguru! Hawapandi, wala hawavuni, wala hawana vichanja wala wekeo jingine. Naye Mungu anawalisha nao. Je? Ninyi hamwapiti ndege pakubwa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, na Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufikiri juu ya kibombobombo: ndege hao hawapandi mbegu, hawavuni, hawana gala wala nafasi yoyote ya kuwekea mavuno, lakini Mungu anawalisha. Ninyi ni wa lazima zaidi kuliko ndege!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Watafakarini kunguru, hawapandi wala hawavuni: hawana pa kuweka akiba wala ghala, na Mungu huwalisha. Ninyi si hora sana kuliko ndege?