Luke 12:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, kila mliyosema gizani, watu watayasikia katika mwanga, na kila mliyonongona faraghani milango imefungwa, yatatangazwa juu ya nyumba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, lolote mlilosema gizani litasikiwa nuruni. Na kile mlichonong’ona masikioni mkiwa kwenye vyumba vya ndani, kitatangazwa juu ya paa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnachokisema sirini kitasemwa mbele za watu. Na mliyonong'onezana katika vyumba vyenu, yatahubiriwa sehemu za wazi ambako kila mtu atasikia.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo, kila mliyosema gizani, watu watayasikia katika mwanga, na kila mliyonong'ona faraghani milango imefungwa, yatatangazwa juu ya nyumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, kila mliyosema gizani, watu watayasikia katika mwanga, na kila mliyonong'ona faraghani milango imefungwa, yatatangazwa juu ya nyumba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, lo lote mlilosema gizani litasikiwa nuruni na kile mlichonong'ona masikioni mkiwa kwenye vyumba vya ndani, kitatangazwa juu ya paa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, lolote mlilosema gizani litasikiwa nuruni. Na kile mlichonong’ona masikioni mkiwa kwenye vyumba vya ndani, kitatangazwa juu ya paa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, yoyote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatatangazwa juu ya dari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, kila mliyosema gizani, watu watayasikia katika mwanga, na kila mliyonongona faraghani milango imefungwa, yatatangazwa juu ya nyumba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maneno yote, mnayoyasema gizani, yatasikiwa mwangani; nalo mnalolinong'oneza masikioni nyumbani, litatangazwa barazani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni hivi maneno yote mutakayosema katika giza yatasikilika muchana kati. Vilevile maneno yote mutakayosema kwa siri ndani ya chumba chenye kufichama, yatatangazwa juu ya paa la nyumba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi yo yote mliyoyasema gizani, yatasikiwa katika nuru: nalo mlilolisema katika sikio la mtu katika vyumba vya ndani litakhubiriwa juu darini.