Luke 12:30 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wote wasiomjua Mungu. Baba yenu anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa mataifa ya duniani husumbuka sana kuhusu vitu hivi vyote, lakini Baba yenu anafahamu kuwa mnahitaji haya yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hayo ndiyo mambo ambayo watu wote wasiomjua Mungu huyafikiria daima. Lakini Baba yenu anajua ya kuwa mnayahitaji mambo haya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa maana hayo yote ndiyo yanayohangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wote wasiomjua Mungu. Baba yenu anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wasiomjua Mungu husumbuka sana kuhusu vitu hivi vyote. Naye Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnavihitaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa mataifa ya duniani husumbuka sana kuhusu vitu hivi vyote, lakini Baba yenu anafahamu kuwa mnahitaji haya yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wote wasiomjua Mungu. Baba yenu anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wamizimu waliomo ulimwenguni ndio wanaoyatafuta hayo yote; lakini Baba yenu amewajua, ya kuwa mnapaswa nayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni wapagani ndio wanaotafutatafuta vitu hivyo vyote. Baba yenu anajua kwamba munahitaji vitu hivyo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana mataifa wa dunia huyatafuta hayo yote, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo.