Luke 12:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uzeni mali yenu mkawape maskini hizo fedha. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, na kujiwekea hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii, wala nondo hawaharibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Uzeni mali yenu mkawape maskini. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, ambapo mwizi hakaribii wala nondo haharibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Uzeni vitu mlivyo navyo, wapeni fedha wale wanaohitaji. Hii ni njia pekee mnayoweza kufanya utajiri wenu usipotee. Mtakuwa mnaweka hazina isiyoisha mbinguni, mahali ambapo wezi hawawezi kuiba na hakuna wadudu wa kuharibu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Uzeni mali yenu mkawape maskini misaada. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, na jiwekeeni hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii, wala nondo hawaharibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uzeni mali yenu mkawape maskini hizo fedha. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, na kujiwekea hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii, wala nondo hawaharibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Uzeni mali zenu mkawape maskini. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, mahali ambapo mwivi hakaribii wala nondo haharibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Uzeni mali zenu mkawape maskini. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, mahali ambapo mwizi hakaribii wala nondo haharibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwizi, wala nondo haharibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Uzeni mali yenu mkawape maskini hizo fedha. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, na kujiwekea hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii, wala nondo hawaharibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uzeni vitu vyenu, mpate ya kuwagawia maskini! Jishoneeni mifuko isiyochakaa ya kuwekea mbinguni limbiko lisilopungua! Tena ndiko, kusikofika mwizi, wala kusikoharibiwa na mende.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muuzishe vitu munavyokuwa navyo, muwasaidie wamasikini. Mujiwekee feza zisizoweza kuwa na upungufu, nayo akiba isiyoweza kumalizika katika mbingu. Kule wizi hawawezi kukaribia wala nondo hawaharibu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.