Luke 12:36 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka harusini, ili wamfungulie mara atakapobisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka karamu ya arusi, ili ajapo na kubisha mlango waweze kumfungulia mara moja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Iweni tayari kama watumishi wanaomngojea bwana wao anayerudi kutoka kwenye sherehe ya harusi. Bwana wao anaporudi na kubisha mlangoni, watumishi huweza kumfungulia mlango haraka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka arusini, ili wamfungulie mara atakapobisha hodi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka harusini, ili wamfungulie mara atakapobisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka kwenye karamu ya arusi, ili ajapo na kugonga mlango waweze kumfungulia mara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka kwenye karamu ya arusi, ili ajapo na kubisha mlango waweze kumfungulia mara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka harusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka harusini, ili wamfungulie mara atakapobisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi mfanane na watu wanomngoja bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, kusudi wamfungulie mlango papo hapo, atakaporudi na kupiga hodi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukuwe kama watumishi wanaomungojea bwana wao arudie kutoka katika karamu ya ndoa, kusudi wakati anapofika na kupiga hodi wamufungulie mulango mara moja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na ninyi kama watu wanaomngojea bwana wao, atakapoondoka arusini, illi akija na kubisha, wamfungulie marra moja.