Luke 12:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni, atawaketisha mezani na kuwahudumia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Heri wale watumishi ambao bwana wao atakapokuja atawakuta wakiwa wanakesha. Amin, nawaambia, atajifunga mkanda wake na kuwaketisha ili wale, naye atakuja na kuwahudumia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Bwana wao atakapoona kuwa wako tayari na wanamsubiri, itakuwa siku ya furaha kwa watumishi hao. Ninawaambia bila mashaka, bwana wao atavaa nguo, atawakaribisha kwenye chakula kisha atawahudumia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni, atawaketisha mezani na kuwahudumia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni, atawaketisha mezani na kuwahudumia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Heri wale watumishi ambao bwana wao atakapokuja atawakuta wakiwa wanakesha. Amin, nawaambia, atajifunga mkanda wake na kuwaketisha ili wale, naye atakuja na kuwahudumia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Heri wale watumishi ambao bwana wao atakapokuja atawakuta wakiwa wanakesha. Amin, nawaambia, atajifunga mkanda wake na kuwaketisha ili wale, naye atakuja na kuwahudumia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni, atawaketisha mezani na kuwahudumia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wenye shangwe ni watumwa wale, ambao bwana atakapokuja atawakuta, wakikesha. Kweli nawaambiani: Atajifunga na kuwaketisha chakulani, naye atakuja kuwatumikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Heri watumishi wale bwana wao atakaowakuta wakikesha wakati anapofika! Kweli ninawaambia: atafunga mukaba wake vizuri na kuwakaribisha kula chakula, na kubakia pale akiwashugulikia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wa kheri watumishi wale ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesba. Amin, nawaambieni, atajifunga, atawaketisha, atakuja kuwakhudumia.