Luke 12:46 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
bwana wake atarudi siku asiyoitazamia na saa asiyoijua; atamwadhibu mtumishi huyo vibaya na kumweka fungu moja na wasioamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wale wasioamini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo bwana wa mtumishi huyo atakuja wakati usiotarajiwa, wakati ambapo mtumishi hajajiandaa. Ataadhibiwa bila huruma na bwana wake na kumpeleka anakostahili, mahali waliko watumishi wengine wasiotii.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
bwana wake atarudi siku asiyoitazamia na saa asiyoijua; atamkatilia mbali na kumweka fungu moja na wasioamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
bwana wake atarudi siku asiyoitazamia na saa asiyoijua; atamwadhibu mtumishi huyo vibaya na kumweka fungu moja na wasioamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
bwana wake yule mtumwa atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. Huyo bwana wake atamkata vipande vipande na kumwekea fungu lake pamoja na wale wasio waaminifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wale wasioamini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
bwana wake atarudi siku asiyoitazamia na saa asiyoijua; atamwadhibu mtumishi huyo vibaya na kumweka fungu moja na wasioamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
bwana wake mtumwa yule atamjia siku, asiyomngojea, na saa, asiyoitambua, kisha atamchangua kuwa vipande viwili, nalo fungu lake atampa pamoja nao wasiomtegemea Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi bwana wa mutumishi yule atakuja siku asiyozania, na saa asiyoijua. Naye atamupiga vikali na kumwazibu sawa na watu wasiokuwa waaminifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bassi, bwana wa mtumwa yule atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande vipande, atampa sehemu yake pamoja na wasioamini.