Luke 12:47 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Yule mtumishi anayefahamu vyema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtumishi huyo alijua kitu ambacho bwana wake alimtaka afanye. Lakini hakuwa tayari kufanya au kujaribu kufanya kile bwana wake alichotaka. Hivyo mtumishi huyo ataadhibiwa sana!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Yule mtumishi anayefahamu vyema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Yule mtumishi anayefahamu vyema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana yule mtumwa aliyeyatambua, bwana wake ayatakayo, asijitengeneze, wala asiyafanye hayo, aliyoyataka, huyo atapigwa fimbo nyingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mutumishi anayejua mapenzi ya bwana wake, lakini anakosa kujiweka tayari na kutofanya sawa na mapenzi ya bwana yule, atapigwa fimbo nyingi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya Bwana wake, asijiweke tayari, wala kutenda mapenzi yake, atapigwa mapigo mengi;