Luke 12:48 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini yule afanyaye yanayostahili adhabu bila kujua, atapigwa kidogo. Aliyepewa vingi atadaiwa vingi; aliyepewa vingi zaidi atadaiwa vingi zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yeyote ambaye hakujua naye akafanya yale yastahiliyo kupigwa, atapigwa kidogo. Yeyote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi; na yeyote aliyekabidhiwa vingi, kwake vitatakiwa vingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini vipi kuhusu mtumishi asiyejua kile ambacho bwana wake anataka? Yeye pia anafanya mambo yanayostahili adhabu, lakini ataadhibiwa kidogo kuliko mtumishi aliyejua alichotakiwa kufanya. Yeyote aliyepewa vingi atawajibika kwa vingi. Hivyo vingi vitategemewa kutoka kwa yule aliyepewa vingi zaidi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini yule afanyaye yanayostahili adhabu bila kujua, atapigwa kidogo. Aliyepewa vingi atatakiwa vingi; aliyekabidhiwa vingi zaidi atatakiwa kutoa vingi zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini yule afanyaye yanayostahili adhabu bila kujua, atapigwa kidogo. Aliyepewa vingi atadaiwa vingi; aliyepewa vingi zaidi atadaiwa vingi zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ye yote ambaye hakujua naye akafanya yale yastahiliyo kupigwa atapigwa kidogo. Ye yote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi na ye yote aliyekabidhiwa vingi kwake vitatakiwa vingi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yeyote ambaye hakujua naye akafanya yale yastahiliyo kupigwa, atapigwa kidogo. Yeyote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi; na yeyote aliyekabidhiwa vingi, kwake vitatakiwa vingi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini yule afanyaye yanayostahili adhabu bila kujua, atapigwa kidogo. Aliyepewa vingi atadaiwa vingi; aliyepewa vingi zaidi atadaiwa vingi zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yule asiyeyatambua alipofanya yapasayo kupigwa atapigwa fimbo chache. Kwani kila aliyepewa mengi, kwake yatatafutwa mengi, naye waliyemwagizia mengi watazidi kumwuliza mengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa ngambo ingine, yule asiyejua mapenzi ya bwana yake, na anayefanya mambo yanayostahili azabu, atapigwa fimbo chache. Kwa maana kila mutu aliyepewa vingi, ataombwa kutoa vingi zaidi; na aliyepewa madaraka mengi, ataulizwa mengi zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na yule asiyejua, nae amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa mapigo machache. Killa aliyepewa vingi kwake huyu vitatakwa vingi: nae waliyemkabidhi vingi, kwake yeye watataka vingi zaidi.